Publications

2018
Serem S. UHAKIKI LINGANISHI WA MBINU ZA LUGHA KATIKA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI NA MKAGUZI WA SERIKALI. Mara Research Journal of Kiswahili - ISSN 2520-0577 [Internet]. 2018;3:15–28. WebsiteAbstract
Makala hii inahakiki kiulinganishi mbinu za lugha kama zilivyotumika katika tamthilia zilizotafsiriwa za Mkaguzi Mkuu wa Serikali (MMS) (Mwakasaka, 1979) na Mkaguzi wa Serikali (MS) (Madumulla, 1999). Mbinu zilizorejelewa ni kama vile chuku, uzungumzi nafsia, kejeli, matumizi ya barua, kinaya, matumizi ya ndoto, kuchanganya ndimi, misemo na nahau. Nadharia ya Uamilifu katika Tafsiri; Mtazamo wa Kuhakiki Matini ilivyopendekezwa na Reiss (1977) iliongoza utafiti huu. Mtazamo huu wa Kuhakiki una mihimili miwili iliyokuwa msingi wa kutekeleza kazi hii, nazo ni; utambuzi wa kuhakikisha kuwa, kuna utoshelevu wa kimaana, kisarufi na kimtindo katika lugha lengwa kwa minajili ya kuuwasilisha ujumbe kwa wasomaji wake na kaida za matumizi ya lugha na uelewa ya kwamba kwa ajili ya mawasiliano, maana ya neno hurejelewa kwa kuhusishwa na maneno mengine yanayohusiana na mada au muktadha wa diskosi inayozungumziwa. Tamthilia za Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Mkaguzi wa Serikali ziliteuliwa kimaksudi. Katika utafiti mwandishi anarejelea maonyesho yote yanayopatikana katika matini pokezi zilizoteuliwa. Ukusanyaji wa data ya makala hii ulifanywa kwa kuzisoma kihakikifu matini zilizoteuliwa, kisha kuchanganua kiulinganishi mbinu za lugha katika kila kitabu. Ilibainika kwamba, kuna tofauti katika matumizi ya mbinu za lugha katika tafsiri ya vitabu; Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Mkaguzi wa Serikali hata kama watafsiri wanashughulikia matini asilia moja. Uwasilishaji wa data ulifanywa kiufafanuzi na matokeo ya uchunguzi huu yatachangia marejeleo yanayohusu tafsiri linganishi.
2017

Pages